HabariPilipili FmPilipili FM News

Kaunti Ya Mombasa Yahimizwa Kuimarisha Sanaa Na Utamaduni Ili Kuvutia Watalii.

Serikali ya kaunti ya Mombasa imetakiwa kubuni mikakati ya kuimarisha Sanaa na utamaduni kama njia moja wapo ya kuvutia wageni wanao zuru humu nchini.

Akiongea katika karakana ya uchongaji vinyago ya Akamba huko Changamwe mkuu wa utamaduni na Sanaa katika kaunti ya Mombasa Hamisi Juma anasema watatembelea sehemu zote zinazoendeleza Sanaa na utamaduni kama vile Kilifi na Kwale.

Juma anasema lengo lao kama kaunti ni kuwasaidia wanachama wa sekta hiyo , ambayo ameitaja kama kiungo muhimu cha utalii.

Show More

Related Articles