HabariPilipili FmPilipili FM News

Wizara Ya Elimu Kuchunguza Visa Vingi Vya Utungwaji Mimba Kwa Watoto Wa Shule.

Licha ya mtihani wa kitaifa wa darasa la 8 kukamilika bila visa vya udanganyifu, waziri wa elimu amina Mohamed ameeleza kusikitishwa na idadi kubwa ya watahiniwa waliojifungua wakati wa mtihani.

Anasema suala hilo linatia wasiwasi katika sekta ya elimu.

Akiongea mapema hapo jana mda mfupi baada ya mtihani wa KCPE kukamilika, Amina amesema watafanya kikao na washikadau wa elimu kujadili jinsi ya kuthibiti visa kama hivyo siku za usoni.

Show More

Related Articles