HabariPilipili FmPilipili FM News

Familia 50 Kupoteza Makao Kutokana Na Mzozo Wa Ardhi Kilifi.

Zaidi ya familia 50 zimo kwenye hatari ya kupoteza makao kufuatia mzozo mkali wa ardhi baina yao na bwenyenye mmoja eneo la Kanamai majengo kaunti ya Kilifi.

Victor Mwaganda ambaye ni mwakilishi wa wadi eneo hilo anasema familia hizo wakiwemo kinamama na watoto wamelazimika kukenya nje kwenye baridi , kwa hofu ya kukabiliwa na polisi pamoja na watu wanaotumwa  na bwenyenye huyo kubomoa nyumba zao.

Mwakilishi huyo wa wadi amekashifu maafisa wa polisi kwa kile amekitaja kutumiwa na bwenyenye huyo kuwahangaisha wakazi, licha ya kesi ya mzozo huo kuwepo kortini na hata wenyeji kuishi eneo hilo kwa zaidi ya miaka 30.

Juhudi zetu za kuongea na maafisa wa polisi eneo hilo, kujua hali halisi bado hazijafaulu.

Show More

Related Articles