HabariMilele FmSwahili

Raila Odinga na Gideon Moi wamtembelea Kalonzo kumfariji kufuatia kifo cha babake

Kinara wa NASA Raila Odinga na mwenzake wa  chama cha KANU  Gedion Moi wamemtembelea kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka  mtaani Karen  hapa Nairobi kumfariji kufuatia kifo cha babake Peter Musyoka Mairu siku ya jumapili.Raila ameelezea masikitiko  akisema ni jambo rahisi kumpoteza mzazi.Anasema mrengo wa NASA unasimama na Kalonzo wakati huu wa majonzi.Kwa upande  wake  Seneta Moi amewasilisha rambi rambi la babake rais mustaafu Daniel Moi anayesema alikuwa mwandani wa karibu wa Mzee Mairu.

Show More

Related Articles