HabariMilele FmSwahili

Spika wa bunge la kaunti ya Homabay Elizabeth Ayoo atimuliwa

Spika wa bunge la kaunti ya Homabay Elizabeth Ayoo ametimuliwa kupitia kura yenye utata iliyopigwa mchana wa leo.Naibu wa spika Evans Marieba ameongoza mkao ulioopitisha kura hiyo ambayo tayari imekosolewa na kupiziliwa mbali na baadhi ya wawakilishi wadi wakiongoziwa na Ruth Obura, wanaosema mkao wa kujadili hoja ya kumbandua imeandaliwa kinyume na sheria.Aidha wanamtuhumu naibu spika Marieba kwa kuenda kinyume na kanuni za bunge hilo kwa kuruhusu kupigwa kura hiyo bila kumpatia nafasi spika huyo kujitetea huku pia wakidai idadi iliyokuwa bungeni wakati wa kura hiyo haikutosha.Wanasema kuwa spika huyo hakupewa fursa ya kujitetea kabla ya kujadiliwa kwa hoja ya kumtimua.

Show More

Related Articles