HabariMilele FmSwahili

Kidero apata afueni baada ya EACC kukomesha ukaguzi wa mali yake

Aliyekuwa gavana wa Nairobi Dkt Evans Kidero amepata afueni baada ya mahakama kuu kuamuru tume ya EACC kukomesha ukaguzi wa mali yake. Jaji Hedwig Ogudi ameiagiza EACC kusubiri uamuzi atakaotoa juma lijalo kuhusiana na suala hilo. Hii ni baada ya Dkt Kidero kupitia wakili James Orengo kupinga mahakamani uchunguzi unaoendeshwa na EACC dhidi yake akiutaja kuwa kinyume na sheria kuhusu masuala yake ya kisiri. Gavana Kidero anakabiliwa na tuhuma za ufisadi kuhusiana na wizi wa shilingi milioni 213 madai ambayo amekana.

Show More

Related Articles