HabariMilele FmSwahili

Mtihani wa KCPE umekamilika bila visa vya udanganyifu asema Amina Mohamed

Hakuna visa vyovyote vya wizi vilivyoshuhudiwa wakati wa mtihani wa KCPE uliokamilika leo. Waziri wa elimu balozi Amina Mohamed anasema ufanisi huo umepatikana kutokana na ushirikiano wa idara pamoja na wizara mbali mbali za kitaifa. Amedhibitisha kuwa maafisa wa mtihani huko Narok wanachunguzwa kufuatia kutoweka kwa karatasi za mtihani jana. Watu wengine wawili wanatarajiwa kushtakiwa mahakamani Kisii kwa kujidai kuwa watahiniwa.Kadhalika waziri Amina ameagiza uchunguzi wa ongezeko la visa vya watahiniwa waliojifungua wakati wa mtihani huo na kuchukuliwa hatua madhubuti kuvidhibiti.

Show More

Related Articles