HabariPilipili FmPilipili FM News

Watahiniwa Wa KCPE Wakamilisha Mtihani Wao Leo.

Mtihani wa kitaifa wa darasa la nane KCPE hatimaye umekamilika rasmi hii leo kote nchini.

Akiongea katika gereza la wanawake Lang’ata huko Nairobi ambako watahiniwa watatu wamemkamilisha mtihani wao wa KCPE, waziri WA elimu AMina Mohamed amesema zoezi hilo limekamilika bila visa vya wizi wa mtihani kushuhudiwa.

Amina anasema pia masuala mengine yanayohusiana na uhalifu wa mitihani yamepungua kwa asilimia kubwa ikilinganishwa na miaka ya nyuma.

Amepongeza ushirikiano baina ya asasi za serikali kufanikisho zoezi hilo, na kutaka ushirikiano huo uendelezwe katika mitihani ya kitaifa ya kidato cha nne itakayoanza rasmi wiki ijayo.

 

Show More

Related Articles