HabariPilipili FmPilipili FM News

Wawakilishi Wadi Wanafaa Kuheshimiwa Asema Sakaja.

Ipo haja  ya  wawakilishi  wadi kote nchini  kuheshimiwa kwani ndio viungo muhimu katika serikali za ugatuzi.

Huo ni usemi wake mwenyekiti wa  kamati ya leba katika bunge la seneti Johnston Sakaja.

Anasema  baadhi ya maspika katika mabunge ya kaunti wamekua wakiwafinyilia wawakilishi wadi, hatua inayowafanya kushindwa  kutekeleza majukumu yao kwa wananchi.

Sakaja amesema bunge la  seneti litashirikiana na wawakilishi wadi kuona kuwa  wanaendesha  shughuli zao vyema  mashinani.

Show More

Related Articles