HabariPilipili FmPilipili FM News

Mbunge Wa Voi Atoa Onyo Kwa Wazazi Wakati Wa Likizo.

Wito umetolewa kwa wazazi kaunti ya Taita Taveta kufuatilia mienendo ya watoto wao kwa  ukaribu wakati huu wanaanza  likizo ndefu ya Disemba.

Mbunge wa Voi Johnes Mlolwa ameonyesha kusikitishwa na idadi kubwa ya watoto wa kike wenye umri mchanga , ambao wamefanyia mtihani wao wa KCPE hospitalini kutokana na wao kuwa wajawazito.

Amewataka wazazi kuwashughulisha wanao na kazi za nyumbani kuhakiili kusaidia kuwaepusha na masuala ya uhalifu.

 

Show More

Related Articles