HabariPilipili FmPilipili FM News

Mwanafunzi Aliyetoweka Wakati Wa Mtihani Apatikana Kichakani.

Mwanafunzi  mmoja  wa shule ya msingi ya Mavirivirini huko kinango kaunti ya kwale aliyetoweka  hapo jana baada ya mtihani wa KCPE  kuanza, hatimaye amepatikana  salama akiwa amejificha msituni usiku wa kuamkia leo.

Kamishna wa kaunti ya kwale Karuku Ngumo anasema mwanafunzi huyo Ndaro kombo kutoka kijiji cha kaluweni  huko kasemeni amepatikana mwendo wa saa nne usiku na  chifu  wa eneo hilo.

Ngumoa anasema mwanafunzi huyo amekubali kuendelea na mtihani wake baada ya kupewa  ushauri mwafaka  na chifu huyo.

 

 

 

 

 

 

Show More

Related Articles