HabariPilipili FmPilipili FM News

Chebukati Afika Mbele Ya Kamati Ya Bunge Ya Uhasibu.

Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Wafula Chebukati anahojiwa na kamati ya uhasibu bungeni kuhusu sakata ya shilingi bilioni sita zilizotumiwa visivyo wakati wa uchaguzi.

Chebukati akihojiwa ametakiwa kutoa taarifa zote kuhusiana na masuala ya ununuzi wa vifaa vya uchaguzi uliopita ambapo wabunge hao walidai kuwa Chebukati ana uoga kutoa taarifa kuhusiana na mikutano yote waliyofanya kama tume ya uchaguzi wakati wa uchaguzi mkuu uliopita.

Hata hivyo Chebukati amesema hakuna lolote wanaloogopa kufichua lakini kuna masuala ambayo ni ya siri na hayafai kutolewa.

 

 

 

Show More

Related Articles