HabariMilele FmSwahili

Mutua apata afueni kufuatia kutupiliwa mbali kesi ya ufisadi dhidi yake

Kesi ya ufisadi iliyokuwa inamwaandama gavana wa Machakos Alfred Mutua kuhusiana na ununuzi wa magari kaunti hiyo imeondolewa mahakamani. Hii ni baada ya ofisi ya mkurugenzi wa mashtaka Noordin Hajji na tume ya kukabiliana na ufisadi EACC kuiambia mahakama  ya Machakos kuwa hazinui kuendelea na kesi hiyo. Gavana Mutua alikuwa anakabiliwa na madi ya kukiuka sheria kwa kununua magari 15 ya Subaru na moja aina ya toyoya Landcruiser kinyume na taratibu za kisheria mwaka wa 2013.

Show More

Related Articles