HabariMilele FmSwahili

Idadi kubwa ya watahiniwa waripotiwa kuifanya mitihani hiyo hospitalini

Idadi kubwa ya watahiniwa wameripotiwa kuifanya mitihani hiyo hospitalini. Katika eneo la Tinderet kaunti ya Nandi mtahiniwa mmoja amejifungua saa chache kabla ya kuuanza mtihani huo. Mshirikishi wa kanda ya Riftvalley, Mwongo Chimwanga  akidhibitisha mtahiniwa anakabidhiwa karatasi zake hospitalini ili pia naye afanye mtihani wake.Hali sawia imeshuhudiwa kaunti ya Kwale, ambapo mwanafunzi katika shule ya Voroni naye amejifungua dakika chache kabla ya kuanza somo la hesabu. Watahiniwa wengine 2 wanaifanyia mitihani yao hospitalini. Mmmoja akiwa mjamzito katika hospitali ya Karatina na mwingine akiwa mgonjwa katika hospitali ya Embu. Mkurugenzi wa elimu eneo hilo Peter Magere, anasema mikakati inawekwa kuhakikisha wanashiriki mtihini huo.Kaunti ya Nyandarua, waziri wa ugatuzi Eugene Wamalwa aliyeshuhudia kuanza mitihani hiyo, amedhibtisha watahiniwa 2 wataifanya mtihani wao hosptalini baada yao kuugua

Show More

Related Articles