HabariPilipili FmPilipili FM News

Maribe Aachiliwa Kwa Dhamana.

Mahakama kuu jijini Nairobi imemwachilia kwa dhamana ya shilingi milioni moja mwanahabari Jacque Maribe ambaye anakabiliwa na shtaka la mauaji ya mfanyibiashara Monica Kimani.

Akitoa uamuzi huo hii leo jaji wa mahakama kuu ya Milimani jijini Nairobi James Wakiaga amesema sababu zilizotolewa na upande wa mashtaka zakutaka Maribe kutoachiliwa kwa dhamana hazikua na uzito huku akizingatia ombi la Maribe kuwa ni mzazi wa mtoto mmoja hivyo anahitaji kumwangalia mwanawe kwa ukaribu wakati kesi hio ikiendelea.

Aidha jaji wakiaga ametoa maagizo kwa Maribe akisema kwa kipindi chote cha kesi haruhusiwi kuonekana akisoma habari kwenye runinga wala kufanya habari yoyote ambayo inahusiana moja kwa moja na kesi hio.

Wakati huohuo mahakama hio imemnyima dhamana mpenziwe Maribe Joseph Irungu ikisema imezingatia maombi ya upande wa mashtaka kuwa huenda akatatiza ushahidi wa kesi hio hivyo anafaa kuzuiliwa mpaka uchunguzi wa kesi hio utakapo kamilika

Jaji Wakiaga pia ametoa agizo la kuendelea kutibiwa kwa Irungu wakati kesi hio itakapokua ikiendelea mahakamani.

Show More

Related Articles