HabariMilele FmSwahili

Katibu mkuu wa muungano wa wauguzi Seth Panyako aachiliwa huru

Katibu mkuu wa muungano wa wauguzi nchini Seth Panyako pamoja na wakuu wawili wa muungano huo wameachiliwa huru kwa bondi ya shilingi elfu 50 kila mmoja. Hii ni baada ya Panyako  pamoja na wakuu wengine wawili wa muungano huo kupinga madai ya kupanga mkutano haramu na kutatiza amani. Wawili hao walikamatwa jana kwa madai ya kupanga mgomo wa wauguzi katika hospitali kuu ya Kenyatta. Hakimu  mkuu wa mahakama ya Milimani Francis ameagiza kesi hiyo kutajwa tarehe 12 Novemba na  kusikiluizwa sikilizwa tarehe 3 Disemba.

Show More

Related Articles