HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta atoa hakikisho la kuondoka mamlakani atakapokamilisha muhula wake

Rais Uhuru Kenyatta ametoa hakikisho la kuondoka mamlakani atakapokamilisha muhula wake wa uongozi wa taifa mwaka wa 2022. Rais amepuuza madai kuwa shinikizo la mageuzi ya katiba nchini kwa sasa linanuiwa kumwezesha kusalia mamlakani. Katika mahojiano na shirika la habari la CNN rais Kenyatta amesema serikali yake  imeweka mkakati wa kuhakikisha kuwa taifa linasalia dhabiti na kuepuka mgogoro sawia na ulioshuhudiwa baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Vile vile amesema azma yake kuu ni kukuza uchumi wa nchi na kuhakikisha kuwa Kenya ni kituo kikuu cha kibiashara barani Afrika.

Show More

Related Articles