HabariMilele FmSwahili

Ndege ya kwanza kutoka Nairobi kuelekea Marekani yatua katika uwanja wa JF Kennedy

Ndege ya kwanza ya Kenya Airways  ya kutoka Nairobi kuelekea  New York Marekani imewasili katika uwanja wa ndege wa  JF Kennedy huko Marekani.Ndege hiyo ilibeba abiria 234 ilitua dakika chache  baada ya saa nane baada ya kucheleweshwa kwa dakika 30.Ndege hiyo ilikuwa na rubani 4 akiwemo mkenya kapteni Joseph Kinuthia pamoja na wafanyikazi wengine 12.Ujumbe wa Kenya umeongozwa na waziri wa masuala ya kigeni  Balozi Amina Mohammed.

Show More

Related Articles