HabariMilele FmSwahili

Katibu mkuu wa muungano wa kitaifa wa wauguzi Seth Panyako akamatwa

Katibu mkuu wa muungano wa kitaifa wa wauguzi Seth Panyako amekamatwa na kuzuiliwa katika kituo cha polisi kwenye hospitali kuu ya Kenyatta. Maafisa wa polisi wamemtia mbaroni Panyako kwa madai kupanga kuongoza maandamano ya wauguzi kwenye hospitali hiyo. Kulingana na afisa wa mawasilanio katika KNH Simon Ithai, Panyako alivamia hospitali hiyo na kuwaagiza wauguzi kugoma pasi na kufuata utaratibu wa kisheria. Ithai pia amewaonya wauguzi hao zaidi ya 2700 kuwa watachukuliwa hatua kwa kushiriki mgomo wa muungano wasio kuwa wanachama.

Show More

Related Articles