HabariMilele FmSwahili

Sonko atozwa faini ya shilingi nusu milioni kwa kufeli kufika mbele ya kamati ya seneti

Gavana wa Nairobi Mike Sonko ametozwa faini ya shilingi nusu milioni kwa kufeli kufika mbele ya kamati ya seneti ya hesabu za umma alivyoagizwa. Hii ni mara ya tatu kwa Gavana Sonko kukosa kufika mbele ya kamati hiyo inayoongozwa na seneta wa Homabay Moses Kajwang. Gavana Sonko ameagizwa kujiwasilisha tarehe 3 Disemba kujibu masuali yaliyoibuliwa na mkaguzi mkuu wa serikali Edward Ouko kuhusiana na matumizi ya fedha katika serikai ya kaunti ya Nairobi.

Show More

Related Articles