K24 TvNEWSSwahiliVideos

KESI YA MATANGAZO: Mbunge Ayub Savula angali kizuizini kwa wizi wa Ksh 122M

Huku Mbunge wa Lugari Ayub Savula na afisa mkurugenzi wa shirika linalosimamia matangazo ya kibiashara ya serikali, Dennis Chebitwey pamoja na aliyekuwa katibu katika wizara ya mawasiliano na teknolijia Sammy Itemere wanaposalia kuzuiliwa,

Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai bado wanazidi kuwasaka wake wawili wa Savula, Melody Gatwiri na Hellen Jepkor Kemboi kwa tuhuma za kupanga kuilaghai serikali zaidi ya shilingi milioni 122, katika idara ya serikali inayohusika na matangazo ya kibiashara.

Hii ni kufuatia idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji kwamba kuna ushahidi wa kutosha wote 23 kutoka wizara ya mawasiliano na teknolojia. Watuhumiwa wote watawasilishwa mahakamani Jumatatu.

Show More

Related Articles