HabariMilele FmSwahili

Obado aahidi kuzingatia masharti ya mahakama baada ya kuachiliwa huru hapo jana

Gavana wa Migori Okoth Obado ameahidi kuzingatia masharti ya mahakama baada ya kuachiliwa huru hapo jana. Katika taarifa Obado ameishukuru mahakama  kuu kwa kukubali ombi lake la kuachiliwa kwa  dhamana.Anasema sasa ataweza kuwahudumia wenyeji wa Migori bila vikwazo.Obado kadhalika amewashukuru waakilishi wadi, wafanyikazi wa kaunti hiyo na wafuasi wake kwa kusimama naye.

Show More

Related Articles