HabariMilele FmSwahili

Mtu 1 afariki baada ya jengo la orofa 8 kuporomoka mapema leo Malindi

Mtu mmoja amefariki  baada ya jengo la orofa 8 kuporomoka mapema leo katika eneo la barani huko Malindi kaunti ya Kilifi. Watu takribani 10 wameokolewa wakiwa hai. Kamanda wa polisi Kilifi Fredrick Ochieng amedhibitisha polisi pamoja na wale wa shirika la msalaba mwekundu wamekuwa wakijitahidi kuwaokoa watu wanaoripotiwa kuzikwa kwenye vifusi vya jengo hilo.Kulingana na  mshirikishi wa shirika la msalaba mwekundu eneo hilo Hassan Mussa jengo hilo ambalo lilikuwa linaendelea kujengwa limeanguka saa 11 asubuhi hii. Wenyeji wanadai mkasa huo umetokea wakati mvua kubwa ikishuhudiwa katika eneo hilo kwa siku tatu mfululizo.

Show More

Related Articles