HabariMilele FmSwahili

Naibu rais atuma risala za rambi rambi kwa familia ya marehemu Jane Kiano

Viongozi mbali mbali wanaendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa mwenyekiti wa chama cha maendeleo ya wanawake Jane Kiano. Katika risala zake za rambi rambi kwa familia ya marehemu, Naibu rais William Ruto amesema Kenya imempoteza kiongozi shupavu na aliyetetea masuala ya jinsia kwa ujasiri. Naibu rais amesema marehemu Bi Kiano atakumbukwa kwa jitihada zake katika kuboresha elimu ya wasichana na maisha ya kina mama nchini kupitia miradi mbali mbali ya maendeleo. Bi Kiano ameaga dunia usiku wa kuamkia leo katika Nairobi Hospital akipokea matibabu ya saratani ya mapafu.

Show More

Related Articles