HabariPilipili FmPilipili FM News

Mtu Mmoja Afariki Baada Ya Nyumba Kuporomoka Malindi.

Mtu mmoja amjethibitishwa kufariki na wengine kujeruhiwa mapema leo baada ya nyumba moja kuporomoka mjini Malindi.

Shughuli za uokozi zinaendelea kwa sasa kuwatafuta watu wanaohofiwa kukwama ndani ya vifusi vya jengo hilo.

Akithibitisha tukio hilo kamanda wa polisi kaunti ya kilifi Fredrick Ochieng, anasema watu 8 kufikia sasa wameokolewa na kukimbizwa hospitalini kupokea matibabu. Kulingana na Ochieng watu kadha wanaaminika kukwama chini ya vifusi vya jengo hilo.

Walioshuhudia wanasema mkasa huo umetokea saa kumi na moja asubuhi eneo la barani kaunti ya kilifi.

Show More

Related Articles