HabariPilipili FmPilipili FM News

Kiunjuri Akutana Na Kamati Ya Kilimo Bungeni.

Waziri wa kilimo Mwangi Kiunjuri hii leo amekuwa na wakati mgumu kujibu maswali ya wabunge akiwa mbele ya kamati ya bunge kuhusu kilimo.

Kiunjuri ametakiwa kueleza kamati hiyo endapo wakulima wa mahindi wamelipwa pesa zao  au la.

Akijieleza mbele ya kamati hiyo, Kiunjuri amesema kufikia sasa shilingi bilioni 9.41 zimelipwa kwa wakulima, na kwamba ni shilingi bilioni 1.2 pekee ndio zilikuwa bado hazijalipwa.

Aidha anasema malipo ya shilingi bilioni 1.4 kwa wakulima 152 yangali yanachunguzwa, sawia na shilingi milioni 429 kwa wakulima 74, ambazo hazilingani na kiwango cha mahindi wakulima hao wanacho dai kupeana kwa bodi ya nafaka nchini NCPB.

Show More

Related Articles