HabariPilipili FmPilipili FM News

Mvua Yatatiza Usafiri Na Biashara Mombasa.

Huku mvua ikiendelea kunyesha katika sehemu nyingi eneo hili la pwani, wafanyibiashara wengi wamelazimika kufunga biashara zao kutokana na makali ya mvua hiyo, huku wengine wakionekana kuathirika kiafya.

Aidha baadhi ya barabara pia zimefurika maji na kutatiza usafiri katika baadhi ya sehemu za mji.

Wakazi tulioweza kuzungumza nao wameiomba serikali ya kaunti kurekebisha miundo misingi ya kupitisha maji taka ili kutatua halin hiyo.

Upande wa biashara wafanyibiashara wa reja reja  wamelazimika kufunga biashara zao, wakisema imeshindikina kuendea bidhaa sokoni kufuatia mvua kubwa inayonyesha .

Show More

Related Articles