HabariMilele FmSwahili

Gavana Obado bado azuiliwa katika gereza la Industrial Area Nairobi

Gavana wa Migori Okoth Obado bado anazuiliwa katika gereza la Industial Area Nairobi baada ya kukosa waadhamini watakaohakikisha anaachiliwa huru. Obado ambaye aliachiliwa jana na mahakama ya milimani kwa dhamana ya shilingi milioni 5 na wadhamini 2 wa kiasi sawia inaarifiwa bado hajapata fedha hizo. Rodgers Sagana mmoja wa mawakili wa gavana Obado,ameiambia Milele Fm wakati huu wanaendelea na mchakato wa kusaka fedha hizo za kugharamia wadhamini 2.Sagana hata hivyo anasema iwapo juhudi zao zitakosa kuzaa matunda leo, huenda basi gavana Obado akakesha tena katika gereza la Industrial Area hadi kesho.

Show More

Related Articles