HabariPilipili FmPilipili FM News

Watoto Wa Akasha Wakiri Mashtaka Ya Ulanguzi Wa Dawa Za Kulevya Marekani.

Watoto wawili wa marehemu Akasha, Baktash Akasha na Ibrahimu Akasha wamekiri mashtaka sita dhidi yao ya ulanguzi wa dawa za kulevya katika mahakama ya New York nchini Marekani.

Uamuzi huo umetolewa na kushuhudiwa na mchunguzi mkuu wa kesi hio kutoka humu nchini Hamisi Masa.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter idara ya upelelzi nchini DCI imethibitisha wawili hao walikiri mashtaka ya ulanguzi wa dawa za kulevya pamoja na ufisadi.

Ikumbukwe wawili hao walitiwa mbaroni Januari 28 mwaka jana na baadae walisafirishwa hadi Marekani nakuzuiliwa huku kesi dhidi yao ikiendelea kuskizwa.

Kulingana na sheria za nchini Marekani kosa la ulanguzi wa dawa za kulevya hukumu yake ni kifungo cha maisha.

 

Show More

Related Articles