HabariPilipili FmPilipili FM News

Gavana Kingi Ahimiza Viongozi Kuzingatia Maendeleo.

Gavana wa kaunti Kilifi Amason Kingi amewataka wanasiasa wanaozungumzia   kura ya maoni kuipa nafasi kamati iliyotwikwa jukumu  la kuleta utangamano nchini , kufuatia mwafaka wa rais Kenyatta na kinara wa NASA Raila Odinga  ikamilishe ripoti yake ya kuchukua maoni kutoka kwa wananchi.

Kingi amesema ripoti hiyo ndio itatoa mwelekeo wa aidha kufanyike  kura ya maoni au la.

Kingi amewataka viongozi kuwajibikia maswala  yanayolenga kuboresha maisha ya wananchi  kiuchumi sawia na kulitilia mkazo swala la ajenda nne za maendeleo nchini kama zilivyoainishwa na rais Kenyatta.

 

Show More

Related Articles