HabariPilipili FmPilipili FM News

SRC Kutathmini Ubora Wa Wafanyikazi Kabla Ya Kuajiriwa.

Tume ya makadirio ya mishahara ya wafanyikazi wa umma nchini SRC imezindua mpango wa vituo vya kutathmini ubora wa wafanyikazi wa umma kabla ya kuajiriwa.

Mwenyekiti wa tume hiyo Lin Mengich anasema Vituo hivvyo vitakavyojulikana kama (assessment centre) vitakuwa na jukumu la kutambua tajiriba, uwezo na viwango vya elimu pamoja maadili kwa wafanyikazi watakao ajiriwa katika sekta mbali mbali za umma.

Mengich anasema kubuniwa kwa vituo hivyo kutasaidia taasisi za umma kuajiri wafanyikazi wake kwa kuzingatia maadili, akisema Kenya imekuwa ikipoteza asilimia 30% ya pato lake kutokana na ufisadi.

Show More

Related Articles