HabariMilele FmSwahili

Wafuasi wa Gavana Obado wapongeza kuachiliwa kwake

Wafuasi wa gavana wa Migori Okoth Obado wanaendelea kusherehekea uamuzi wa mahakama kuu kumwachilia huru kwa dhamana ya shilingi milioni 5.Wafuasi hao waliomiminika nje ya mahakama ya Milimani hapa jijini Nairobi wamepongeza uamuzi huo wakiutaja kuwa wa haki. Wamesema shughuli muhimu zilikwama wakati gavana huyo akiwa kizuizini. Huko Migori shamra shamra zimepamba moto wafuasi wa gavana huyo wakijiandaa kumpokea kwa shangwe. Baadhi yao hata hivyo wametoa wito kwake kushirikiana na polisi katika kuitendea haki familia ya Sharon Otieno.

Show More

Related Articles