HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta atia saini mswada wa bajeti ya ziada ya shilingi bilioni 47.25

Rais Uhuru Kenyatta ametia saini mswada wa bajeti  ya ziada ya shilingi bilioni 47.25 kiwango kikubwa kikitengewa mpango wa makaazi bora kwa wakenya.Mswada huo umewasilishwa kwa rais na  spika wa bunge la taifa Justine Muturi.Shilingi bilioni 21  zimetengewa mpango wa makaazi mojawapo ya nguzo nne muhimu za maendeleo.Idara ya mahakama imefaidi pia kwa kutengewa shilingi bilioni 1.5 ile ya ujenzi ikipewa bilioni 1.9.Shilingi bilioni 2 zimetengewa ufadhili wa mipango ya kuendeleza utalii.

Show More

Related Articles