HabariMilele FmSwahili

Serikali yawekeza nusu bilioni kujenga kituo cha kitaifa cha wanafunzi wenye ulemavu

Serikali imewekeza shilingi nusu bilioni kujenga kituo cha kitaifa kitakachowahudumia wanafunzi wenye ulemavu. Katibu wa elimu Dkt Belio Kipsang anasema kituo hiki kitawasaidia zaidi ya wanafunzi elfu 250 wenye ulemavu kupokea mafunzo maalum na yanayoambatana na ulemavu wao. Kulingana na Kipsang asilimia 60 ya wanafunzi hawa wanasomea shule za kawaida hali ambayo ni kinyume na haki zao aidha Kipsang amewataka wadau katika sekta ya elimu kuunga mkono juhudi za serikali kuboresha na kuimarisha masomo haya

Show More

Related Articles