HabariMilele FmSwahili

Wazazi na watahiniwa washauriwa kutonunua karatasi zinazodaiwa kuwa za mitihani ya kitaifa

Wazazi pamoja na watahiniwa wameendelea kushauriwa kutokubali kununua karatasi zinazodaiwa kuwa za mitihani ya kitaifa. Katibu msimamizi katika wizara ya usalama Patrick Ntutu anasema karatasi halisi za mtihani zimehifadhiwa chini ya ulinzi mkali. Akihutubu eneo la Emarti, Trans Mara Magharibi, Ntutu amepuuzilia mbali karatasi zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii na kukariri kujitolea kwa serikali kuhakikisha uadilifu kwenye mitihani hiyo.

Show More

Related Articles