HabariPilipili FmPilipili FM News

Disko Matanga Yatajwa Kuchangia Katika Upotovu Wa Maadili.

Hisia mseto zinazidi kuibuka miongoni mwa wakazi wa kaunti ya Kilifi kuhusiana na suala la Disko Matanga almaarufu siniriche.

Wakizungumza katika kikao cha washikadau wa elimu mjini Kilifi wakazi wanasema disko matanaga ndio chanzo cha maovu katika jamii ikiwemo kuzorota kwa elimu, mimba na ndoa za mapema miongoni mwa wasichana wadogo.

Wakiongozwa na Joseph Jira wakazi hao wamewataka viongozi katika kaunti hiyo kutoa suluhu la kudumu ili kukomesha itikadi hiyo.

Kwa upande wake mbunge wa Kilifi Kaskazini Owen Baya amesema  suala la disko matanga limekuwa kivutio kukubwa cha biashara mbali mbali, na itakuwa vigumu endapo serikali itahusisha maafisa wa usalama katika kusitisha suala hilo.

Show More

Related Articles