HabariPilipili FmPilipili FM News

Wavuvi Watahadharishwa Dhidi Ya Mawimbi Makubwa Baharini.

Tahadhari imetolewa kwa wavuvi kuwa wangalifu katika bahari hindi kutokana na mawimbi makubwa na upepo mkali unaoshuhudiwa.

Akiongea na meza yetu ya habari katibu wa kongamano la wavuvi wa pwani Anwar Abae, amethibitisha kuwepo hali mbaya ya hewa baharini, ambayo inakadiriwa kuwa huenda ikachukua zaidi ya siku 7 hadi kumi.

Abae anasema kulingana na mabadiliko ya hali ya anga duniani , kwa sasa ni vigumu kupata utabiri wa uhakika baharini, na hivyo kuwarai wavuvi kukwepa kuingia katika maji makuu kwa usalama wao.

Kulingana naye kuna hatari ya mawimbi makubwa na upepo mkali unaovuma kwa kasi.hata hivyo anasema kufikia sasa bado hakujaripotiwa mkasa wowote wa mtu kuzama au boti kuharibiwa.

Show More

Related Articles