HabariPilipili FmPilipili FM News

Wanaozidi Kutumia Mifuko Ya Plastiki Waonywa Vikali.

Mamlaka ya usimamizi wa mazingira nchini NEMA imetahadharisha wenyeji wa Mombasa  wanaojihusisha na biashara ya mifuko ya plastiki kabla hawajafikiwa na mkono wa sheria.

Onyo hii imetolewa na Steve Wambua mkurugenzi wa mamlaka hiyo kaunti ya  Mombasa akiwahutubia wanahabari katika kituo cha polisi cha Central hapa Mombasa akithibitisha kwamba usiku wa kuamkia jana takriban vipande Milioni 1 vya bidhaa hizo bandia zilinaswa na maafisa wa mamlaka ya NEMA wakishirikiana na polisi baada ya kupata habari kutoka kwa wanainchi.

Show More

Related Articles