HabariMilele FmSwahili

Mwanamke 1 ajitia kitanzi katika mtaa wa Juakali Machakos

Polisi huko Machakos wanachunguza kisa cha mwanamke anayedaiwa kujitia kitanzi katika eneo  mtaa wa Juakali huko Mavoko mapema leo.Naibu kamishna sehemu hiyo David Juma anasema mwili wake uligunduliwa na jirani zake ukiwa na mshipi shingoni anaoshukiwa kuutumia kujiua.Anasema hakuwacha ujumbe wowote wa kuelezea sababu za kujitoa uhai.Kisa hiki kinajiri siku moja baada ya kamisha wa Machakos Abdulahi Galgallo kulalamikia ongezeko la watu wanaojitia kitanzi kaunti hiyo.

Show More

Related Articles