HabariPilipili FmPilipili FM News

Wakulima Wapinga Bei Ya Mahindi Iliyopendekezwa Na Serikali.

Huenda bei ya unga wa mahindi ya shilingi 75 kwa mfuko wa kilo 2 ikapanda baada ya wakulima hasa katika eneo la Uasingishu kupinga bei ya kuuza mahindi kwa wasagaji iliyopendekezwa na serikali.

Mkuu wa chama cha wakulima eneo hilo Kipkorir Menjo, anadai wakulima watapata hasara kubwa iwapo watashurutishwa kuwauzia wasangaji mahindi yao kwa shilingi 1,400 kwa gunia.

Ameitaka serikali kuitisha kikao cha dharura na wakulima kupata utatuzi kwa suala hilo.

Show More

Related Articles