HabariMilele FmSwahili

Washukiwa 2 wa ujambazi wajisalimisha kwa polisi Nyeri

Polisi kaunti ya Nyeri wanawazuilia watu wawili wanaodaiwa kuwa washukiwa wakuu wa uhalifu. Hii ni baada yao kujisalimisha katika makao makuu ya idara ya jinai. Washukiwa John Githinji na Joseph Kang’ethe wanasema waliamua kujisalimisha kwa makundi ya kutetea haki za binadamu kabla ya kuelekea katika idara ya jinai kwa kuhofia usalama wao.Naye mkuu wa idara ya jinai eneo hilo Jonah Kirui amedhibitisha washukiwa watahojiwa kabla ya kufikishwa mahakamani.

Show More

Related Articles