HabariMilele FmSwahili

Mahakama yawaachilia huru kwa bondi ya milioni 5 wamiliki wa basi la mauti Fort Tenan Kericho

Washukiwa wawili wa mauaji ya zaidi ya watu 50 waliohusika katika ajali ya Fort tenan kaunti ya Kericho wameachiliwa huru  kwa bodi ya shilingi milioni 5 kila mmoja.Wakiwa mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya Molo Samwel Wahome wawili hao mmiliki wa basi la Homeboys Bernard Ishihindu na Cleophas Shimanyula maneja wa kampuni ya Western Cross Express iliyokuwa ikisimamia basi hilo wamekana kuhusika na mauaji hayo na utokuwa na kibali cha kusafiri usiku. Kadhalika wamekana madai kuwa basi hilo lilihudumu bila bima.

Show More

Related Articles