HabariPilipili FmPilipili FM News

Washikadau Katika Sekta Ya Utalii Waomboleza Kifo Cha Mahinder Singn Vohra.

Risala za rambi rambi zinaendea kutolewa  baada ya kifo cha Mahinder  Singn Vohra aliyekuwa mwenyekiti wa mikahawa ya za sarova kenya. Mahinder aliangamia kwenye ajali hiyo iliyofanyika maeneo ya KILIMA KIU kaunti ya Makueni , pamoja na mkewe, mwanawe wa kike na mke wa mwanawe Js Vorha aliyefariki kwenye ajali ya barabarani mwaka jana huko maeneo ya Amboseli ,akiwa kwenye msafara wa gari za mashindano ya mbio za afrika mashariki Safari Classic Rally.

Mwenyekiti wa shirikisho la Utalii nchini Mohammed Hersi na mkurugenzi mkuu wa mkahawa wa Diani Reef Titus Kangang’i wanasema kifo cha Mahinder ni pigo kubwa kwa sekta ya Utalii na umiliki wa mikahawa ya watalii nchini.

Mwanawe Mahinder, aliyepata  majeraha madogo  mwilini anaendelea kupokea matibabu katika hospitality a Sultan Hamud level five  jijini Nairobi, huku miili ya waliofariki ikihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha HOSPITALI YA Machakos level five Hospital

Show More

Related Articles