HabariMilele FmSwahili

Mfungwa azua kizaa zaa baada ya kumvamia askari magereza na kinyesi Eldoret

Kizaa zaa kimeshuhudiwa katika kituo cha polisi cha Central mjini Eldoret baada ya mfungwa mmoja aliyekuwa akisubiri kufikishwa mahakamani kumshambulia kwa kinyesi afisa wa polisi. Mfungwa huyo pia alipaka ukuta na eneo la kuwapokea wageni  kinyesi hicho hali iliyopelekea wakazi waliokuwa wakisuburi kuhudumiwa kuondoka kituoni. Iliwabidi maafisa wa zima moto wa Uasingishu kuitwa kusawazisha hali hiyo. Juhudi zetu za kutaka kuzungumza na OCPD wa Eldoret Magharibi Zacharia Bitok kuhusiana na kisa hizi hazikufaulu.

Show More

Related Articles