HabariMilele FmSwahili

Wabunge Ali Raso na Chachu Ganya wakamatwa

Wabunge Ali Raso wa Saku na Chachu Ganya wa Hoor Kaskazini wamekamatwa. Wawili hao wanahusishwa na mapigano ya kiukoo ambayo yamepelekea vifo vya wenyeji 14 kufikia sasa. Inaarifiwa wakati huu wanasafirishwa kuletwa hapa Nairobi ili kuandikisha taarifa katika makao ya jinai DCI kuhusu wanachofahamu katika mapigano hayo. Kukamatwa kwao kunawadia huku viongozi kaunti hiyo wakitangaza kuungana kukabili mapigano yanayozuka kila mara eneo hilo

Show More

Related Articles