HabariPeople DailyPilipili FmPilipili FM News

Washukiwa Wa Uwindaji Haramu Watiwa Mbaroni Katika Kaunti Ya Kwale.

Maafisa wa shirika la hifadhi ya wanyamapori nchini KWS  kwa  ushirikiano wa maafisa  wa polisi  wa kituo cha Diani kaunti ya kwale,  wamefanikiwa kuwanasa washukiwa wawili wa uwindaji haramu  katika eneo la Mvindeni huko Diani eneo la Msambweni .

Washukiwa hao  wamepatikana na pembe tatu za ndovu zilizo na uzani wa kilo 19, zenye thamani ya shilingi milioni 1.9.

Akithibitisha tukio hilo kamishna wa kaunti ya Kwale Karuku Ngumo anasema wawili hao SURA ALI PANGO  na mwenzake Juma Ali Mwamadi,  wametiwa mbaroni  baada  ya  polisi kupashwa habari na wananchi,  wakati wwili hao wakijaribu kusafirisha pembe hizo kwa kutumia pikipiki .

Wawili hao  wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo kufunguliwa mahtaka ya kumiliki pembe haramu za ndovu.

Show More

Related Articles