HabariPilipili FmPilipili FM News

Mtihani Wa KCSE Kungoa Nanga Hii Leo.

Wanafunzi wa kidato cha nne wanatarajiwa kuanza mtihani wao wa kitaifa KCSE  hii leo.

Usalama umeimarishwa katika shule za upili kote nchini ili kuthibiti visa vyovyote vya wizi wa mtihani huo .

Watahiniwa wanatarajiwa kuanza na mtihani wa Practicals ambao utakamilika tarehe mosi novemba , kabla ya mitihani mingine kuanza novemba 5 na kukamilika novemba 29.

Kwa kipindi cha wiki mbili zijazo watahiniwa pia watakalia mitihani ya  lugha za French, German , Arabic , lugha za ishara humu nchini , mapishi pamoja na sayansi ya masuala ya kinyumbani.

Itakumbukwa kuwa mapema hapo jana rais Kenyatta alitoa onyokali kwa wanaopania kuiba mtihani akisema hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Show More

Related Articles