HabariPilipili FmPilipili FM News

Siungi Mkono Pendekezo La Kura Ya Maoni Dori Asema.

Mwenyekiti  wa wabunge wa  pwani  ambaye pia  ni mbunge wa Msambweni   Suleiman Dori anasema kuwa haungi mkono pendekezeko la kuwepo kwa kura za maoni inayolenga kuifanyia mageuzi  katiba.

Dori aliyekuwa akizungumza katika sherehe za mashujaa  hapo jana zilizofanyika katika shule ya msingi ya Jomo kenyatta  huko Msambweni ,amesema kuwa mageuzi hayo ya katiba  hayatamfaidi mwananchi wa kawaida.

Dori anasema kuwa uchumi wa nchi  umedorora kwa kiwango kikubwa  hivyo zoezi hilo la kura ya maoni linalenga kumkandamiza mwananchi  kwani linahitaji kima kikukbwa cha fedha .

Show More

Related Articles