HabariMilele FmSwahili

Rais Kenyatta kuongoza maadhimisho ya Mashujaa Day kesho Kakamega

Rais Uhuru Kenyatta ataongoza taifa katika maadhimisho ya siku ya mashujaa hapo kesho mjini Kakamega.Ni maadhimisho ambayo pia yatahudhuriwa na rais wa Namibia Hage Geingob kama mgeni mashuhuri.Tayari maandalizi yote yamefikia kilele katika uwanja wa Bukhungu, katibu mkuu wa usalama wa ndani Karanja Kibicho akitoa hakikisho la kuwepo usalama wa kutosha.Amesema lango kuu la uwanja huo litafunguliwa mapema kuruhusu sherehe hizo kuandalwia chini ya ratiba iliyowekwa.

Show More

Related Articles