HabariMilele FmSwahili

Usalama waimarishwa Kakamega kabla ya siku kuu ya Mashujaa day kesho

Usalama umeimarishwa mjini kakamega chini ya saa 24 kabla ya Kenya kuadhimisha siku kuu ya Mashujaa hapo kesho. Kamishna wa kaunti Kakamega Anne Ng’etich amewahakikishia wenyeji pamoja na wageni wanaoendelea kumiminika mjini huko usalama wao. Kadhalika umma utaruhusiwa kuingia katika uwanja wa Bukhungu kuanzia saa 11 asubuhi huku rais Uhuru Kenyatta akiratibiwa kufika saa nne asubuhi.Wakati uo huo rais wa Namibia Hage Geingob, amewasili nchini ambapo atakuwa mgeni mwalikwa katika maadhimisho ya kesho ya siku kuu ya Mashujaa. Geingob, ambaye wakati huu anafanya mashauriano na mwenyeji wake rais Uhuru Kenyatta amekagua gwaride la heshima  katika ikulu ya Nairobi. Ziara ya rais  Geingob, nchini inatazamiwa pia kuimarisha uhusiano katika nyanja mbali mbai baina ya Kenya na Namibia.

Show More

Related Articles